Urusi yaendelea kuchukua udhibiti wa maeneo ya Ukraine
30 Juni 2025Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi pamoja na wanablogu wanaofuatilia vita hivyo.
Hata hivyo taarifa hiyo haijathibitishwa na vyanzo kutoka Ukraine wala Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Mara kadhaa Urusi imekuwa ikitaja kuwa tayari kusaini mkataba wa amani lakini ikiitaka Ukraine kujiondoa kikamilifu katika mikoa minne ambayo Urusi iliinyakua kinyume cha sheria.
Hayo yanajiri wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul amewasili hivi leo mjini Kyiv katika ziara ambayo haijatangazwa na yenye lengo la kudhihirisha kuwa Ujerumani inaendelea kuunga mkono mapambano ya Ukraine.
Wadephul anatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha.