Urusi: Wanajeshi wa kigeni watashambuliwa wakiletwa Ukraine
6 Septemba 2025Matangazo
Putin ametoa kauli hiyo baada ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kusema kuwa maelfu yaaskari hao wanaweza kuwekwa nchini Ukraine kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani.
Wakati huo huo waziri mkuu wa jimbo la Bavaria la Ujerumani, Markus Söder, ametilia mashaka wazo la kuwapeleka wanajeshi wa NATO nchini Ukraine kuwa sehemu ya dhamana ya usalama wa nchi hiyo.
Mapema wiki hii kinachojulikana kuwa Muungano wa Hiari unaoongozwa na Ufaransa na Uingereza, ulisema nchi 26 za magharibi zipo tayari kupeleka wanajeshi ili kuwezesha kusimamisha vita na kuleta amani kati ya Urusi na Ukraine.
Baada ya kutolewa tangazo hilo, Ujerumani imesema haiko tayari kutoa kauli ya uhakika juu kushiriki katika hatua kama hiyo.