MigogoroUlaya
Mashambulizi ya droni yarindima Ukraine, Urusi
26 Januari 2025Matangazo
Taarifa hiyo imesema droni nane zilidunguliwa katika mkoa wa Ryazan, sita katia mkoa wa Kursk na moja kwenye mkoa wa Belgorod usiku wa kuamkia Jumapili. Gavana wa Ryazan amesema hakukuwa na majeruhi katika mashambulizi hayo ya hivi karibuni lakini bado mamlaka zinafanya tathmini ya uharibifu uliotokea.
Soma zaidi: Urusi yadai kuingia katikati mwa mji wa kimkakati mashariki mwa Ukraine
Kwa upande wake Ukraine imebainisha kwamba imezidungua droni 50 kati ya 72 kutoka Urusi usiku wa kuamkia leo. Jeshi la anga la Ukraine limesema droni tisa kati ya zilizorushwa zilipoteza mwelekeo na kupotea. Jeshi hilo na mamlaka za Kiraiabado hazijatoa ripoti kuhusu uwepo wa majeruhi au uharibifu uliosababishwa na mashambulizi hayo.