SiasaUrusi
Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa wa kivita
20 Juni 2025Matangazo
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema zoezi hilo la sita kwa mara nyingine lilifanyika kwenye mpaka wa Ukraine na Belarus.
Hakuna idadi rasmi iliyotolewa lakini kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari inaaminika kwamba pande zote zilikabidhi idadi sawa ya mateka.
Kwenye mazungumzo ya nchini Uturuki, Ukraine na Urusi zilikubaliana juu ya kubadilishana wafungwa wa kivita wenye umri wa chini ya miaka 25. Kwa mujibu wa taarifa ya rais wa Urusi, Vladimir Putin nchi hizo mbili zimeshabadilishana wafungwa wa kivita zaidi ya 900. Hata hivyo. Ukraine haijathibitisha idadi hiyo.