SiasaUrusi
Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa wa kivita
14 Juni 2025Matangazo
Urusi na Ukraine zimebadilishana wafungwa wa kivitaleo, ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo zinazopigana wakati wa mazungumzo ya mjini Istanbul, mapema mwezi huu.
Urusi imeikabidhi Ukraine miili ya askari 1,200 waliouawa wakati wa vita vinavyoendelea, ingawa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi vimesema kuwa Moscow haikupokea mwili wowote wa askari wake kutoka Kyiv.
Wizara ya ulinzi ya Urusi haikutoa taarifa pia ni wafungwa wangapi wamehusika katika zoezi la mabadilishano, ila imechapisha vidio ikionyesha askari wake walioshikilia bendera za Urusi kabla ya kupanda basi.
Wafungwa wa Urusi wapo nchini Belarus wanakopatiwa matibabu kabla ya kurejeshwa nchini.