Urusi na Ukraine washambuliana kwenye pwani za Bahari Nyeusi
24 Julai 2025Matangazo
Jeshi la Urusi lilifanya shambulizi kubwa la ndege zisizo na rubani katika bandari ya Odesa ya Ukraine, na kuwajeruhi takriban watu wanne, na kusababisha moto na uharibifu katika eneo la kihistoria ambalo ni sehemu ya urithi wa dunia wa shirika la UNESCO.
Kwa mujibu wa gavana wa Mkoa wa huo, Oleh Kiper, mashambulizi hayo yameathiri pia soko maarufu la Pryvoz mjini Odesa.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, kupitia mtandao wa Telegram amesema Urusi ilirusha droni 103 na makombora manne katika mashambulizi hayo ya usiku. Naibu Waziri Mkuu, Oleskiy Kuleba, alieleza kuwa mashambulizi hayo yalilenga miundombinu ya kiraia kama bandari, vituo vya usafiri, na maeneo ya makazi.