Migogoro
Urusi na Ukraine kufanya mazungumzo Istanbul
2 Juni 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani Marco Rubio na kujadili juu ya matarajio ya mazungumzo hayo.
Baada ya simu hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema katika taarifa kwamba Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito wa kuendelea na mazungumzo hayo ya moja kwa moja kati ya Urusi na Ukraine ili kufikiwa kwa suluhisho la mzozo huo wa zaidi ya miaka mitatu.
Hata hivyo, wakati nchi hizo zikijiandaa kwa mazungumzo ya amani hii leo, hapo jana pande zote mbizi ziliripoti mashambulizi ya kijeshi.