Mazungumzo ya Urusi na Marekani kufanyika wiki ijayo
6 Aprili 2025Kulingana na shirika la habari la TASS la Urusi, Dmitriev amesema licha ya matumaini ya kufufuka kwa mazungumzo kati ya mataifa hayo hapana shaka kuwa bado kuna maadui wengi wa Urusi ndani ya serikali ya Marekani.
Ameyasema hayo siku kadhaa baada ya kufanya ziara mjini Washington wiki iliyopita. Ziara hiyo ni ya kwanza kwa afisa wa ngazi ya juu wa Urusi nchini Marekani tangu ilipoivamia Ukraine mwezi Februari mwaka 2022.
Soma zaidi: Wajumbe wa Marekani na Urusi wakutana Riyadh kutafuta suluhu ya vita vya Ukraine
Wakati huohuo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya kuwa Urusi imeongeza mashambulizi ya anga dhidi ya nchi yake. Ameyasema hayo baada ya Urusi kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya kyiv kwa kutumia makombora na droni kulingana na Waziri Mkuu msaidizi wa Ukraine. Hayo yanajiri wakati Urusi ikisema kuwa imekiteka kijiji kimoja katika mkoa wa Summy ndani ya Ukraine.