Urusi na Marekani zimefanya mazungumzo kuhusu Ukraine
19 Februari 2025Matangazo
Kulingana na vyombo vya habari vya Urusi, Peskov amesema kulikuwa na mazungumzo hayo wakati wa mkutano wa jana kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio pamoja na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.
Hata hivyo Peskov ameongeza kuwa uamuzi kuhusu suala hilo hauwezi kufanyika nchini Urusi ama Marekani.
Soma pia:Marekani na Urusi zakubaliana kumaliza vita Ukraine
Katika kile kinachoonekana kama juhudi za kumtenga Rais Zelensky, Urusi imemtaja kuwa kiongozi asiye halali na imekuwa ikitoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi ambao huenda ukasababisha kuondolewa kwake madarakani.
Ukraine imekuwa chini ya sheria ya kijeshi tangu uvamizi wa Urusi huku chaguzi za bunge na urais zikifutiliwa mbali na shughuli za kisiasa kuzuiwa.