MigogoroMashariki ya Kati
Urusi na China zalaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran
19 Juni 2025Matangazo
Wakati huo huo, mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza watakutana siku ya Ijumaa mjini Geneva kwa mazungumzo ya nyuklia na mwenzao wa Iran Abbas Araghchi, huku nchi hizo za magharibi zikitoa pia wito wa kupunguza uhasama katika mzozo huo kati ya Israel na Iran.
Hata hivyo, mataifa mbalimbali duniani yameendelea kuwaondoa raia wao kutoka katika mataifa hayo hasimu kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi katika kila upande.