Urusi na Belarus kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi
12 Agosti 2025Wizara hiyo imemnukuu Meja Jenerali Valery Revenko akisema kwamba lengo la mazoezi hayo ni kupima uwezo wa kujikinga wa mataifa hayo mawili pamoja na kuhakikisha usalama wa kijeshi na utayari wa kukabiliana na uchokozi wa aina yoyote.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alitoa onyo mapema mwaka huu bila ya kutoa maelezo zaidi, kwamba Urusi inajitayarisha kushambulia kutoka Belarus katika msimu huu wa joto chini ya kisingizio cha kufanya mazoezi ya kijeshi.
Belarus yasema inaungana na Urusi kwenye luteka za pili za kijeshi
Wiki iliyopita Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, alisema ameamua kubadilisha sehemu ya kufanyia mazoezi hayo ya pamoja mbali na magharibi mwa Belarus inayopakana na mataifa mengi ya Ulaya kufuatia masuala ya usalama nchini Poland na mataifa ya Baltic.