Urusi: Mazungumzo kuhusu Ukraine bila sisi ni kazi bure
20 Agosti 2025Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, amesema Urusi inapendelea dhamana za uhakika kwa Ukraine na akapendekeza kuwa zinaweza kujumuishwa kwenye rasimu ya makubaliano ambayo yalijadiliwa kati ya pande zinazozozana mjini Istanbul mnamo 2022.
Marekani, Ulaya zajadili dhamana ya ulinzi kwa Ukraine
Matamshi ya Lavrov yameonyesha hitaji la Urusi kwa mataifa ya Magharibi kujihusisha nayo moja kwa moja katika masuala ya usalama kuhusu Ukraine na Ulaya, jambo ambalo inasema yamekata kufanya.