Urusi kupeleka ujumbe kwa mazungumzo ya amani Istanbul
30 Mei 2025Haya yamesemwa leo na msemaji wa ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov.
Kikosi cha Urusi kitakachoshiriki kwenye mazungumzo hayo ni kile kile kilichoshiriki mazungumzo ya awamu ya kwanza kilichoongozwa na waziri wa zamani wa utamaduni, Vladimir Medinskiy.
Mkuu wa ujumbe wa Ukraine Rustem Umerov amesema nchi yake haipingi mazungumzo ila ingependa kuuona mpango wa amani wa Urusi kwanza.
Ila muda mfupi uliopita, mshauri mmoja mkuu wa Rais Volodymyr Zelenskiy amesema kuwa Ukraine, iko tayari kwa kufanyika tena mazungumzo ya amani ya moja kwa moja na Urusi, mnamo Jumatatu.
Andrii Yermak katika taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya rais wa Ukraine amesisitiza uwepo wa rasimu ya mpango wa amani wa Urusi.
Ukraine na washirika wake wa Umoja wa Ulaya wamekuwa wakiituhumu Urusi kwa kujikokota katika kutafuta amani huku ikiendelea kunyakua ardhi zaidi ya Ukraine.