Urusi inajivuta kujibu pendekezo la usitishaji vita
13 Machi 2025Zelensky kupitia ujumbe wake aliouandika kwenye mitandao ya kijamii, amelalamika kwamba kwa bahati mbaya ulimwengu haujasikia jibu lolote kutoka Urusi, kuhusiana na pendekezo la usitishaji vita.
Malalamiko ya Zelensky ameyatowa chini ya kiwingu cha ziara ya mjumbe maalum wa Marekani Steven Witkoff nchini Urusi ambako atakuwa na mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo.
Soma pia:Mawaziri wa G7 wajadili usitishaji mapigano Ukraine
Kiev iliridhia kusitisha vita kwa siku 30, katika mazungumzo yaliyofanyika Jeddah,Saudi Arabia, japo wawakilishi kutoka Moscow hadi sasa wameonesha kutilia mashaka pendekezo hilo.
Kadhalika mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tajiri kiviwanda za kundi la G7 wanakutana Canada kujadili kuhusu pendekezo hilo la usitishaji vita Ukraine.