SiasaUrusi
Urusi: Hatujapata mualiko wa mazungumzo ya amani
4 Aprili 2025Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, aliyenukuliwa na shirika la habari la serikali la TASS mjini Moscow, akisema hadi sasa hakuna dalili zozote.
Peskov alikuwa akijibu kauli ya Rais wa Finland, Alexander Stubb, aliyependekeza kwamba ama Ufaransa au Uingereza iwe wawakilishi wa Ulaya katika mazungumzo na Moscow.
Soma pia: Ukraine na Urusi zaendelea kutupiana lawama
Kufikia sasa, Urusi na Marekanizimekuwa zikifanya mazungumzo ya kusitisha vita bila kuyahusisha mataifa ya Ulaya wala Ukraine yenyewe katika jitihada za kumaliza vita hivyo.