Ureno yaomboleza kufuatia ajali iliyoua watu 15 mjini Lisbon
4 Septemba 2025Ureno inafanya maombolezo ya kitaifa ya siku moja hivi leo, baada ya ajali kutokea jana katika mji mkuu Lisbon iliyosababisha vifo vya watu 15.
Mamlaka haijatoa taarifa kuhusu watu waliokufa ama watu 23 ambao polisi wanasema walijeruhiwa katika ajali hiyo inayoelezwa kuwa mbaya kabisa kuwahi kutokea katika mji mkuu huo katika historia ya karibuni.
Idara za utoaji huduma za dharura mjini Lisbon zimesema takriban watu 15 waliuawa na 18 kujeruhiwa Jumatano moja wakati gari la kifahari la reli maarufu kwa jina Elevador da Gloria lilipoacha njia.
Katika taarifa yake, Taasisi ya Kitaifa ya huduma za Dharura za kitabibu imesema watu watano kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya akiwemo mtoto mmoja na wengine ni wageni.
Kulingana na idara za utoaji wa huduma za dharura, waathiriwa wote wamepatikana kutoka kwa mabaki ya gari hilo.