Upinzani Uturuki waitisha maandamano nje ya bunge
23 Aprili 2025Matangazo
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CHP, Ozgur Ozel, amesema atahutubia nje ya bunge wakati nchi hiyo ikiadhimisha leo siku ya uhuru wa taifa.Soma pia:Kamata kamata yaendelea Uturuki dhidi ya maelfu ya waandamanaji
Ozel amewaambia wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi leo alasiri akisisitiza kwamba raia ndiyo wenye mamlaka ya taifa hilo.
MeyaSoma pia: Kiongozi wa upinzani Uturuki amtembelea Meya aliye gerezani wa mji wa Istanbul aliyekamatwa mwezi mmoja uliopita, kwa tuhuma za rushwa, Ekrem Imamoglu, ambaye ni mgombea urais wa chama cha CHP mwaka 2028, pia ametowa mwito akiwa gerezani wa kutaka waturuki washiriki maandamano hayo.