SiasaBurundi
Upinzani: Uhaba wa mafuta Burundi utaathiri uchaguzi ujao
4 Aprili 2025Matangazo
Muungano huo unaofahamika kama "Burundi Bwa Bose" yaani Burundi ya Wote umesema katika taarifa yake kwamba uendeshwaji wa uchaguzi unatia wasiwasi kwani wagombea hawawezi kuwafikia wafuasi wao kutokana na ukosefu wa mafuta.
Taifa hilo dogo la Afrika Mashariki ambalo linakabiliwa na matatizo ya kiuchumi na linalotegemea uagizaji wa mafuta kutoka nje, limeshuhudia uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo muhimu kwa zaidi ya miaka miwili.
Soma pia: Warundi wengi wakabiliwa na uhaba mkubwa wa mahitaji ya msingi
Kiongozi wa muungano huo Patrick Nkurunziza amesema Burundi inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi kutokana na "maamuzi ya kutowajibika ya serikali na usimamizi mbaya wa masuala ya umma".