Upinzani Sudan kusini wasema uko chini ya mashambulizi mapya
22 Aprili 2025Juba
Upinzani nchini Sudan Kusini umevishtumu vikosi vya serikali kwa kuzishambulia moja ya ngome zake za kijeshi katika jimbo la Ikweta ya Kati leo katika wakati ambapo makubaliano yao tete ya kugawana madaraka yanaendelea kusambaratika.
Jeshi la Sudan Kusini lauteka tena mji muhimu kutoka kwa wanamgambo
Kwenye chapisho katika mtandao wa Facebook, msemaji wa chama pinzani Lam Paul Gabriel, amesema Jeshi la Sudan KusiniSSPDF leo asubuhi limelishambulia eneo la Panyume.
Gabriel amesema mapigano bado yanaendelea na maelezo yatafuata baadaye.
HRW: Sudan Kusini ilitumia silaha za moto kuwauwa watu 60
Taarifa nyingine iliyotolewa na Gabriel, imesema kwa kukabiliwa na mfululizo wa mashambulizi kwenye maeneo yake, kamanda wa vikosi vya upinzani Luteni Jenerali Peter Thok Chuol, amevielekeza vikosi vyake vyote vya SPLA-IO kuwa macho na kujilinda pamoja na raia walio chini ya maeneo yao.
Mgawanyiko waibuka ndani ya chama cha SPLM-IO, Sudan Kusini
Jimbo la Ikweta ya Kati linaloijumuisha Juba, liligawanywa katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali na vikosi vya upinzani chini ya makubaliano ya kugawana madaraka ya 2018 ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano.