Tume ya Uchaguzi Kenya IEBC imeikosoa hatua ya muungano wa upinzani NASA ya kutaka kuweka kituo sambamba cha kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu ujao na kuitaja hatua hiyo kuwa usaliti na hujuma kwa tume huru iliyo na mamlaka ya kipekee kisheria kutangaza matokeo.