Mshauri wa kiuchumi wa Muungano wa upinzani NASA, David Ndii, ameibua mjadala mkali baada ya kusema katika mahojiano ya televisheni kuwa wakati umewadia kwa sehemu nyengine za Kenya kujitenga.
Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Githu Muigai, amekemea vikali maoni hayo akisema yataligawa taifa hata zaidi kwa misingi ya kikabila. Caro Robi amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Herman Manyora, na kwanza amemuuliza mtizamo wake kuhusu suala hilo la baadhi ya maeneo kujitenga ili kujitawala.