UNICEF yaonya kuhusu ukame yasema watoto wamo hatarini
20 Juni 2025Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto, UNICEF, limetahadharisha kuhusu ukame uliotengenezwa makusudi katika Ukanda wa Gaza wakati ambapo mifumo ya maji ya eneo hilo ikiendelea kuporomoka.
UNICEF imeonya kwamba watoto wataanza kufa kwa kiu kutokana na hali ya ukame inayoendelea huko Gaza. Msemaji wa shirika hilo, James Elder, amefahamisha kwamba ni asilimia 40 tu ya vifaa vya kuzalisha maji ya kunywa ndivyo vinavyoendelea kufanya kazi. Amesema hali katika Ukanda wa Gaza ipo chini sana ya viwango vya dharura katika suala la maji ya kunywa.
Wakati huo huo,UNICEFpia imeripoti juu ya ongezeko la asilimia 50 la watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka 5 waliolazwa kwa ajili ya matibabu yanayohusiana na utapiamlo kutoka mwezi Aprili hadi mwezi Mei huko Gaza, ambako watu nusu milioni wanakabiliwa na njaa.