UNICEF: Watoto wa Sudan wako hatarini
5 Agosti 2025Matangazo
Hayo yameelezwa Jumanne na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF.
Mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan, Sheldon Yett amesema watoto hawana uwezo wa kupata maji salama, chakula, na huduma za afya.
Yett amesema utapiamlo umekithiri, na watoto wengi wamekonda vibaya. Kulingana na UNICEF, kutokana na kupunguzwa ufadhili hivi karibuni, washirika wengi wa Khartoum na kwengineko wamelazimika kupunguza matumizi yao, hali inayochangia watoto kufa kwa njaa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Wakimbizi, UNHCR na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yanakabiliwa na moja ya mizozo mibaya ya fedha katika miongo kadhaa, uliosababishwa na hatua ya Marekani na mataifa mengine wafadhili, kupunguza ufadhili misaada ya kigeni.