MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
UNHCR: Watu 800,000 waikimbia Kongo kutokana na mzozo
5 Machi 2025Matangazo
Takriban watu 61,000 kati ya hao wamekimbilia Burundi kuomba hifadhi, nchi ambayo imepokea idadi kubwa ya wakimbizi kufuatia mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Kongo na kundi la waasi wa M23.
Uungwaji mkono wa Rwanda kwa kundi hilo, umeiwezesha M23 katika miezi ya hivi karibuni kuchukua udhibiti wa maeneo mengi ya mashariki mwa DRC yenye utajiri wa madini na kupelekea maelfu ya watu kuyahama makazi yao na kusababisha kile ambacho UNHCR imekitaja kuwa moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu duniani.
Ujerumani imesema itasitisha msaada mpya kwa Rwanda kutokana na mashambulizi ya kundi la M23 mashariki mwa nchi hiyo ambapo kulingana na watalaamu wa Umoja wa Mataifa, waasi hao wanasaidiwa na wanajeshi wa Rwanda.