JamiiAfghanistan
UN yawataka Taliban waondoe marufuku ya elimu kwa wasichana
18 Machi 2025Matangazo
Baraza hilo la Umoja wa Mataifa limelaani pia matukio ya ugaidi yanayofanyika nchini Afghanistan na kutoa wito wa kuongezwa kwa juhudi za kuboresha hali ya kiuchumi na kiutu nchini humo.
Soma pia:ICC yataka hati ya kuwakamata viongozi wawili wa Afghanistan
Baraza hilo limeuongeza muda wa mpango wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini humo ufahamikao kama UNAMA hadi Machi 17, mwakani.
Wanamgambo wa Taliban walichukua mamlaka mwaka 2021 baada ya wanajeshi wa Marekani na jamii ya kujihami ya NATO kuondoka nchini humo, kufuatia miongo miwili ya mapigano.