Umoja wa Mataifa umewapongeza viongozi wa Kenya baada ya kiongozi wa muungano wa Upinzani wa NASA Raila Odinga kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kwa mara ya kwanza na kufikia makubaliano ya kuondowa mvutano wa kisiasa. Pongezi hizo za kimataifa zinachukuliwa vipi na hali halisi ya kisiasa nchini Kenya ikoje?