MigogoroKimataifa
UN yapunguza mipango ya misaada ya kiutu
17 Mei 2025Matangazo
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umepunguza mipango yake ya misaada ya kibinadamu katika mataifa ya Yemen na Somalia, ikiwa ni matokeo ya kupungua maradufu kwa ufadhili kutoka kwa nchi wanachama.
Umoja wa Mataifa umesema hatua hiyo inahatarisha maisha ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni.
Januari mwaka huu, Umoja wa Mataifa uliwasilisha ombi la dola bilioni 2.4 ili kuwasaidia watu milioni 10.5 katika nchi ya Yemen iliyoharibiwa na vita, huku ikikadiria kuwa watu milioni 19.5 ndio wanaohitaji msaada.
Katika wiki za hivi karibuni, mabadiliko sawa na hayo yalitangazwa pia katika mataifa ya Ukraine na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.