SiasaSudan
UN yaonya juu ya kuundwa kwa serikali ya amani nchini Sudan
6 Machi 2025Matangazo
Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kwamba hatua hiyo huenda ikazidisha vita na mgogoro wa hali ya kibinadamu nchini Sudan.
Wanachama wa baraza hilo, jana usiku walitowa tamko la kuonesha wasiwasi wao huku pia wakitowa mwito kwa pande zote kwenye mzozo huo, kusitisha vita mara moja na kujiunga na juhudi za mazungumzo ya kisiasa na kidiplomasia kuelekea hatua ya kutafuta amani ya kudumu katika taifa hilo.
Kwa takriban miaka miwili, jeshi na kundi la RSF wako kwenye vita vilivyosababisha maelfu ya watu kuuwawa na zaidi ya milioni 12 wakiachwa bila makaazi.