UN yaomba dola milioni 900 za msaada kwa Haiti
21 Februari 2025Katika mpango wake wa msaada wa kibinadamu kwa mwaka 2025, Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada OCHA, limesema kuwa hali ya kibinadamu nchini Haiti iliendelea kuzorota mwaka 2024.
OCHA imeongeza kuwa vurugu za silaha zimesababisha mateso yasio kifani hasa miongoni mwa wanawake na watoto.
OCHA pia imesema viwango vya njaa vimezidi kuwa vibaya, huku watu milioni 5.5 kufikia sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, hili likiwa ongezeko la aslimia 11 ikilinganishwa na Machi mwaka 2024, ambapo watu milioni mbili walikabiliwa na dharura ya chakula na wengine 6,000 na baa la njaa.
Marekani yafuta hatua ya kusimamisha msaada wa ujumbe wa Haiti
Katika siku za hivi karibuni, mashambulizi yameongezeka katika mji mkuu Port-au-Prince huku mapigano yakiripotiwa kati ya vikosi vya usalama na makundi yenye silaha.