UN yaitaka Taliban kuondoa vikwazo kwa wanawake Afghanistan
8 Julai 2025Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo limepitisha azimio la Marekani la kuwataka watawala wa Afghanistan wa Taliban kuondoa ukandamizaji wao kwa wanawake na wasichana na vile vile kuondoa mashirika yote ya kigaidi nchini humo.
Azimio hilo lenye kurasa 11 linasisitiza umuhimu wa kutengeneza fursa za kufufua uchumi, maendeleo na ustawi nchini Afghanistan na kuwatolea mwito wafadhili kusaidia kushughulikia hali mbaya ya kiuchumi na mgogoro wa kibinadamu katika taifa hilo.
Tangu walipotwaa madaraka nchini Afghanistan mwaka 2021, Taliban wameweka sheria kali, kupiga marufuku wanawake kutoka kwenye maeneo ya umma na wasichana kutozidi elimu ya darasa la sita.
Itakumbukwa kwamba wiki iliyopita, Urusi ilikuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuitambua serikali ya Taliban.