MigogoroIsrael
UN yapinga ukaliaji wa mabavu wa Israel huko Ukanda wa Gaza
8 Agosti 2025Matangazo
Turk amesema mpango huo "unakwenda kinyume na maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya kukomesha ukaliaji wake mara moja, kufikia makubaliano ya suluhu la madola mawili na haki ya Wapalestina kujitawala."
Badala yake ameitaka Israel kuruhusu ufikishwaji usio na vikwazo wa misaada na Hamas kuwaachilia mateka bila masharti.
Kiongozi wa upinzani nchini IsraelYair Lapid ameutaja uamuzi huo kuwa "janga" litakalochochea majanga mengi zaidi, huku Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akiukosoa kwa kusema ni "makosa" kuidhinisha mipango ya kuikalia Gaza.
Kauli hizi zinafuatia hatua ya mapema leo ya baraza la usalama la Israel kuridhia mpango wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa kuukalia tena kimabavu Ukanda wa Gaza.